Jumapili 25 Oktoba 2026 - 11:25
Kufungwa Mipaka ni ‘Vita vya Kiuchumi’ Dhidi ya Wananchi

Hawza/ Mahdi Amrali, mwenyekiti wa Kambi ya Badr katika Bunge la Iraq, amekosoa vikali uamuzi wa serikali wa kufunga mpaka wa Al-Shaib (Chadhaba) huku akieleza kuwa hatua hiyo inaonesha mkanganyiko katika ufanyaji wa maamuzi, hali inayosababisha moja kwa moja kupanda bei na kuongeza mzigo wa maisha kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Mahdi Amrali, mbunge wa Iraq na mwenyekiti wa Kambi ya Badr, katika taarifa rasmi aliyotoa, alisisitiza kuwa uamuzi wa kufunga njia ya Al-Shaib unaakisi hali ya mkanganyiko na vurugu zilizo wazi katika mchakato wa kufanya maamuzi ya serikali.

Alibainisha kuwa hatua hiyo inachangia moja kwa moja kupanda kwa bei za bidhaa na kuwawekea mzigo mkubwa wananchi wenye kipato cha chini.

Katika taarifa hiyo, Amrali alifafanua kuwa sababu zilizotolewa na serikali za kuhalalisha uamuzi huo, zikidai kuwa njia hiyo “haikidhi vigezo vya kiufundi”, ni kauli zisizo sahihi ambazo hazina uhusiano wowote na hali halisi. Alisisitiza kuwa hakuna kasoro yoyote ya kiufundi au kiutawala inayoweza kuhalalisha kufungwa kwa njia hiyo.

Mbunge huyo wa Iraq pia alibainisha kuwa kuna nia na vipengele vingine vilivyofichika nyuma ya uamuzi huo, ambavyo vinavuka masuala ya kiufundi.

Mwishoni mwa taarifa yake, mwenyekiti wa Kambi ya Badr aliongeza kuwa; njia ya Al-Shaib ni mojawapo ya njia muhimu na za kimkakati kwa uchumi wa taifa. Alieleza kuwa kuchukua hatua za aina hiyo bila tafakuri ya kutosha kunadhuru uwezo wa biashara ya Iraq kushindana katika soko na kudhoofisha uwezo wa wananchi wa kununua bidhaa katika soko la ndani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha